Psalms 146

Kumsifu Mungu Mwokozi

1 aMsifuni Bwana!
Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.


Ee nafsi yangu, umsifu Bwana,
2 cNitamsifu Bwana maisha yangu yote;
nitamwimbia Mungu wangu sifa
wakati wote niishipo.
3 dUsiweke tumaini lako kwa wakuu,
kwa wanadamu ambao hufa,
ambao hawawezi kuokoa.
4 eRoho yao itokapo hurudi mavumbini,
siku hiyo hiyo mipango yao yote hukoma.

5 fHeri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,
ambaye tumaini lake ni katika Bwana, Mungu wake,
6 gMuumba wa mbingu na nchi,
na bahari na vyote vilivyomo ndani yake:
Bwana anayedumu kuwa mwaminifu
milele na milele.
7 hNaye huwapatia haki walioonewa
na kuwapa wenye njaa chakula.
Bwana huwaweka wafungwa huru,
8 i Bwana huwafumbua vipofu macho,
Bwana huwainua waliolemewa na mizigo yao,
Bwana huwapenda wenye haki.
9 j Bwana huwalinda wageni
na kuwategemeza yatima na wajane,
lakini hupinga njia za waovu.

10 k Bwana atamiliki milele,
Mungu wako, ee Sayuni,
kwa vizazi vyote.

Msifuni Bwana.
Copyright information for SwhNEN